Thursday 24 November 2016

How TELEPHONE FARMING works

TELEPHONE

Jinsi telephone farming inavyo fanya kazi.

Mkulima: Juma vipi umewapatia kuku Chakula?
Juma: Ndio nimewapatia na wanaendelea kula;
Ukweli: Hapo umemkumbusha awapatie maanake Alisha pitiwa mambo mengi sana.
Mkulima: Juma vipi Dawa uliwapatia kuku? Na wanaendeleaje sasa?
Juma: Nimewapatia kwa sasa wanaendelea vizuri na wamechangamka sana na wanakula pia
Wewe sasa: Hapo unapata afueni na masaa yanakuendea vizuri
Ukweli: kuku hawajapewa dawa bali ndo umekumbusha awapatie dawa.
Juma: Hallo Mama/Baba, kuku kadhaa hapa hali ni mbaya pamoja na kuwapa dawa naona hali imebadilika na wamejikunyata sana na hawali kabisa.
Mkulima: Wako wangapi hao kuku?
Juma: Wako 9 ambao hali ni mbaya sana,

Hapo ni jioni sana karibia na usiku
Usiku unakuwa mbaya sana kwako maanake kuku wanaumwa sana,

Asubuhi
Mkulima: Vipi Juma hao kuku wanaendelea vipi?
Juma: Hao walio kuwa wanaumwa sana wamekufa ila hawa wengine wanaendelea vizuri kiasi.
Mkulima:Dah, hakikisha unawapatia dawa mapema na chakula.
Juma: Sawa ila tuma pesa ya dawa maanake imekaribia kuisha, chakula chao nacho kinakata kimebakia cha leo mchana pekee, na pia chakula chamimi kula ni cha kuongezwa.
Hahahaa: Pamoja na matatizo yote ila unaombwa pesa, yaani uko kwenye majinzi kuku 6 wameondoka ila unaombwa pesa na unatakiwa kuongeza.
Juma: Kuna wengine wawili wamekufa tena,
Mkulima: Dah
Ukweli: Unaweza kuta hawajafa ila sasa kwa ule muendelezo wa kuumwa ndo na wao wanapata chansi kukupiga.

UPIGAJI
1. Kipindi cha kuku kuumwa ndo kipindi cha kupigwa maanake utakuwa unaambiwa na kuna mwingine kafa
2. Hawana pesa sasa; Jioni unaweza pigiwa simu kuna kuku wanaumwa sana, kesho yake itaambiwa wamekufa, sasa hapo unakuta wameisha enda kuuzwa.

CHAKULA CHA KUKU
3. Msosi wa kuku.Hahaa hapa ndo kuna kupigwa, unaleta mifuko na inauzwa na ukicheza ukileta chakula wao wanakata nusu halafu huko wanaongeza pumba hapo ni endapo wewe usha wapigia mahesabu ya chakula cha kuku kulingana na idadi yao
4. Kama hujawapigia  mahesabu basi ni unapigwa mfuko mzima baada ya siku unaambiwa ongeza chakula.
5. Au kuku watapigishwa pasi ndefu mchana wanaweza wasilishwe ili kufidia kilicho pigwa.
6. Au wanaweza fanya kuwaonjesha tu.

WAKIJUA UNAKUJA SASA JUMA MOSI
1. Utakuta usafi umefanywa, kuku wana msosi wana maji na utawakuta wako bise vibaya mno mabandani yaani hata ukiwasemesha wanakujibu wakiwa bandani,
2. Kuku wanao umwa wanaweza hata fichwa ili uone mambo yanaenda sawa.
3. Utakuta wamepika maharage au mboga za majani kukuzuga
.
UKISHITUKIZA KWENDA BILA WAO KUTARAJIA
1. Hahaaa utakuta kuku hawana maji, hakuna cha msosi, kuku wanaumwa na wako kwenye hatua ya mwisho ya kufa,
2. utawakuta hawapo wako misele mtaani.
3. Au utawakuta wamelala wanakula mziki na hawana habari kabisa
4. Unaweza kutana na kilingi cha watu vijana wa mtaani wote wako hapo na masosi wanagonga.
5. Hahaa unaweza kuta kuku kachinjwa tena ndo wale ulio ambiwa wamekufa.
6. Utakuta mayai ymaekaangwa mbaya, flampeni utakuta inamafuta.

KWA KIFUPI KATIKA HIZI PROJECT IKIWEZEKANA FANYA MWENYEWE, IKISHINDIKANA KABISA NO WAY OUT NDO UWATUMIE HAWA WATU,
Wakenya huwa tunalalmika kazi hakuna, ila tatizo ni sisi wenyewe ndo Vijana kama hao.

No comments:

Post a Comment